
Na BBC Swahili News
Marekani imekanusha vikali taarifa za vyombo vya habari zilizotolewa wiki iliyopita kuwa inajihusisha kisiri na mzozo unaoendelea nchini Somalia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Johnnie Carson, alisema utawala mjini Washington hauna mpango wa kuyafanya mapigano kati ya serikali ya mpito ya Somalia na waasi wa kiislam kuwa mapigano yenye sura ya Kimarekani.
Alikanusha kuwa Marekani imetuma washauri wa kijeshi kusaidia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia ili kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al-Shabab.
Juma lililopita gazeti la The New York Times lilisema wanajeshi maalum wa Marekani wako Somalia kuratibu kampeni za kijeshi dhidi ya kundi la Al-Shabab.
Serikali dhaifu ya mpito ya Somalia imekuwa ikikabiliana na makundi ya upinzani ya kiislam, ambayo yanalengo la kuiangusha serikali hiyo.
No comments:
Post a Comment