Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Mgaya Nicholas, akizungumza na waandhishi wa habari Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu mgomo wa Wafanyakazi unaotarajia kufanyika Mei 5 mwaka huu nchi nzima na kuongeza kuwa Sherehe hizo za mwaka huu mgeni rasmi atakuwa ni Mwenyekiti wao, Ayoub Juma badala ya Raisa Jakaya Kikwete, huku wakitumia sherehe hizo kama sehemu ya kuhamasisha mgomo huo.
Na Herrieth Benny
WAKATI nchi ikiwa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka huu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limeitisha Serikali kwa kusema kuwa litafanya mgomo endelevu kwa nchi nzima hadi kieleweke, huku wakitumia vyema jukwaa la sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) kuhamasisha mgomo huo.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Mgaya Nicholas, alisema kuwa wameamua kuitisha mgomo huo kutokana na Serikali kushindwa kutekeleza mambo muhimu matatu yanayowakabili wafanyakazi hao ambayo.
Aidha Nicholas alisema kuwa, katika sherehe hizo za Mei Mosi, wanatarajia kumualika Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Ayoub Juma, kuwa mgeni rasmi badala ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kuwa wakimualika mara kadhaa na kuahidi kuyafanyia kazi baadhi ya matatizo yao bila mafanikio.
Aliyataja matatizo makuu matatu yanayowakabili kuwa ni, mishahara duni, (kiwango cha chini cha mishahara), kutokuwapo kwa bodi ya mishahara na maslahi duni kwa wafanyakazi.
Nicolas alisema kuwa anaamini kuitishwa kwa mgomo huo utasaidia kuikumbusha Serikali kutatua matatizo yao kwani itakuwa ni pigo takatifu kwa Serikali ya Awamu ya Nne iliyoshindwa kufanya majadiliano na wafanyakazi wa Umma tangu ilipopandisha mishara kwa asilimia 4.1.
“Hatukuridhishwa na kiwango hicho, hivyo Waziri wa Kazi aliunda tume iliyomaliza muda wake Aprili mwaka jana lakini hadi leo hatujui kilichopendekezwa katika ripoti hiyo. Sasa hatujui hiyo ripoti watasomewa Waganda au Wakenya”? alihoji Nicholas.
“ Rais alipokwenda Shinyanga kushiriki Siku ya Wafanyakazi, aliunda Tume ya Bunge kufanya uchunguzi kuhusu kodi kubwa kwa wafanyakazi kwenye mashirika ya pensheni, walipokwenda bungeni hawakutetea wafanyakazi, walitetea posho zao zisikatwe, sasa hawa Wabunge wapo kwa ajili yetu ama kwa ajili ya kutetea maslahi yao? alisema Mgaya.
Aidha Mgaya alisema haoni haja ya kuwa na mifuko mingi ya pensheni kwa nchi masikini kama Tanzania, kwani mifuko hiyo inawaumiza wafanyakazi wa chini wakati vigogo pensheni zao zinakatwa kupitia SPF, ambako mafao yao ni makubwa.
“Kuonyesha msisitizo juu ya hili mwaka huu hatumualiki Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wala Waziri wa Kazi, kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi, badala yao tutamualika Mwenyekiti wa TUCTA, Ayubu Omar Juma, kuwa mgeni rasmi na huko mikoani watakuwa wenyeviti wa vyama”.
“Rais na mawaziri wameshindwa kuwajibika kwetu na wametuchoka na sisi tumewachoka, tumekuwa tukisoma risala za kila aina na kuwakabidhi lakini hazina majibu. Safari hii tutamsomea katibu wetu na vyama vyote 14 vimeridhia kuwapo kwa mgomo huu, utakaofanyika Mei 5 mwaka huu nchini kote” alisema.

No comments:
Post a Comment