Habari za Punde

*KANDA KABONGO ATAMBA LIGI YA KICK BOXING, AIBUKA NA PIKIPIKI













Bondia Fadhili Majia (kulia) akimsukumia konde zito mpinzania wake, Yasin Seleman, wakati wa mchezo wa utangulizi katika Ligi ya Mabingwa wa Mabingwa wa Mchezo wa Kick Boxing, hatua ya nusu fainali na fainali uliochezwa juzi kwenye Ukumbi wa DDC Kondoa Magomeni. Katika Fainali ya mchezo huo, Kanda Kabongo wa Dar es Salaam, aliibuka mshindi baada ya kumchapa mpinzani wake, Hamisi Mwakinyo, wa Tanga na kujinyakulia zawadi ya Pikipiki.












Anthony Mwakapalila (kulia) akimwadhibu mpinzani wake Ally Ramadhan, katika mchezo wa utangulizi wa Boxing. Katika mchezo huo Anthony alishinda kwa KO, raundi ya 4 ya mwisho ya mchezo.

Mtoto Mohamed Majid wa Zanzibar (aliyesimama) akimwangalia mpinzani wake, Anuary Semboko, baada ya kumpeleka chini kwa konde zito wakati wa mchezo wao wa kirafiki.



Watoto, Mohamed Majid wa Zanzibar (kulia) na Anuar Semboko wa Dar es Salaam, wakionyeshana umwamba katika mchezo wa Kick Boxing, ikiwa ni mchezo wa kirafiki wakati wa mchezo wa kumtafuta Bingwa wa Mabingwa wa katika Ligi ya mchezo huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
*HUU ULIKUWA NI MPAMBANO WA KUKATA NA SHOKA WA NUSU FAINALI KUWANIA NAFASI YA KUCHEZA FAINALI.




Charles Hagaya mwakilishi wa Mkoa wa Mwanza (kushoto) akipimana ubavu na Hamis Mwakinyo wa Tanga, katika mchezo wa raund tatu. Katika mchezo huo Hamis alishinda na kuingia fainali na Kanda Kabongo.






Hii si ngoma ya asili bali ni konde zito alilosukuma Hamis (kushoto) na kumpelekea mpinzani wake Charles, chini.
HUU PIA ULIKUWA NI MPAMBANO WA NUSU FAINALI KUELEKEA FAINALI.







Kanda Kabongo (kushoto) akimwadhibu mpinzani wake, Emmanuel Shija, katika mchezo wao wa raundi tatu wa kuwania nafasi ya kucheza Fainali ya mchezo huo, ambapo Kabongo alishinda na kuingia Fainali na kupambana na Hamisi.
HUU ULIKUWA MPAMBANO WA UTANGULIZI WA WANADADA.
Ama kweli mtoto wa nyoka ni nyoka, huyu ni mtoto wa aliyekuwa bondia mahiri Omar Yazidu, Fatuma Yazidu (kushoto) akipimana ubavu na mpinzani wake Sakina Semfuko katika mchezo wa utangulizi wa raundi tatu. Katika mchezo huo Fatuma alishinda kwa KO raundi ya kwanza.
HAWA NAO NI WAPINZANI WA MUDA MREFU KATIKA BOXING NA SASA KATIKA KICK BOXING, WAKITAMBIANA KABLA YA MCHEZO KUANZA.









Pendo Njau (kushoto) akitambiana na mpinzania wake, Frola Malecellah, kabla ya kuanza pambano lao la ubingwa wa kuwania mkanda, ikiwa ni miongoni mwa mapambano ya awali katika Ligi ya Kick Boxing jana.










Pendo Njau (kulia) akichapana na mpinzani wake katika mchezo wa Kick Boxing, Frola Malecella, wakati wa mchezo huo wa kuwania mkanda, likiwa ni kati ya mapambano ya utangulizi wakati wa Fainali ya mchezo huo hatua ya Nusu Fainali na Fainali uliochezwa juzi kwenye Ukumbi wa DDC Kondoa Magomeni Dar es Salaam, ambapo, Kanda Kabongo wa jijini, aliibuka kidedea na kunyakua zawadi ya Pikipiki baada ya kumtwanga mpinzani wake, Hamis Mwakinyo, kutoka Tanga.











Pendo Njau (kushoto) na Frola Malecellah, wakipambana.











Si kwamba amenyanyuliwa na mtu la hasha ni teke zito na mpinzani wake lililompeleka juu wakati wa mchezo huo, Pendo Njau (kulia) na Frola Malecellah.
HUU ULIKUWA NI MCHEZO WA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI.











Moses Golola kutoka Uganda (kulia) akichuana na mpinzani wake wa Tanzania. Katika mchezo huo Golola alishinda na kutwaa ubingwa huo kwa kunyakua mkanda.













Golola akimpeleka chini mpinzani wake kwa konde zito.












Golola akivishwa mkanda mara baada ya kutangazwa mshindi.
HII ILIKUWA NI FAINALI YA MCHEZO HUO WA KICK BOXING.












Kanda Kabongo (kushoto) akichuna na mpinzani wake Hamis Mwakinyo. Katika fainali hiyo, Kabongo aliibuka kidedea na kutwaa Pikipiki.










Hamis akiwa chini baada ya konde zito la mpinzani wake, Kabongo.












Hii si mieleka bali ni Kick Boxing, Kabongo na Hamis wakichuana.










Mchezo huo uliendelea kuwa mkali, kuvutia na wa kusisimua huku kila mmoja akishambulia kwa zamu na kushangiliwa ukumbi mzima. Kabongo (kushoto) na Hamis.












Hamis (Kulia) na Kabongo.












Abdulfatah (kushoto), akikabidhi zawadi ya pili ya mshindi wa fainali hizo, Hamis Mwakinyo.













Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan na Abdulfatah, wakimkabidhi zawadi ya pikipiki, Kanda kabongo, baada ya kushinda fainali hizo.









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.