Habari za Punde

*MATUKIO MBALIMBALI YA WIKIENDI KATIKA PICHA JIJINI DAR

*MUSACCOS WATOA MSAADA WA VYANDALUA MUHIMBILI













Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Agnes Mtawa (kulia) akipokea sehemu ya Vyandarua 100 toka kwaMwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha Wafanyakazi waHospitali hiyo kwa niaba ya Wafanyakazi wenzake, Mussa Matata kwaajili ya akinamama wajawazito na watoto hospitalini hapo, mwishoni mwa wiki ikiwa ni kuunga mkono Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malariaya Zinduka. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya akinamama na Uzazi, Dk. Gelease Kamugisha na Meneja wa Jengo la Wazazi, Amina Mwakuluzo (kulia).

*UZINDUZI WA JUKWAA LA KINAMAMA (ULINGO)

Baadhi ya Wajumbe na kinamama waliojitokeza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake (Ulingo). Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Ras (Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia na Mbunge wa Kawe, Ritta Mlaki, wakishangilia mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.


Mama Salma Kikwete, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake (Ulingo), wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

*UPIMAJI WA SARATANI YA MATITI NA VIRUSI VYA UKIMWI KAWE.



Meneja Huduma ya Muuguzi Mission, wa Hospitali ya Mikocheni, Valentina Msechu (kulia) akitoa maelekezo ya junsi ya kujipima Saratani ya Matiti kwa Mkazi wa Mbezi Mdumbwi jijini Dar es Salaam, Stara Migira, wakati wa zoezi la upimaji wa Virusi vya Ukimwi na Saratani ya Matiti, lililofanyika Kawe jijini jana. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa UWT, Kawe, Hilda Rwebangila, Mama Mlezi, Angellah Kairuki na Katibu, Getrude Mandilindi.




Dokta Sehewa Robert (kulia) kutoka NGO iliyochini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, (Pasada), akimtoa damu kumpima virusi vya Ukimwi Mkazi wa Kawe jijini, Mwanaidi Jafari, wakati wa zoezi hilo la upimaji virusi na saratani ya matiti lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake (UWT) Kawe kwa ushirikiano na mlezi wao, Angellah Kairuki, lililofanyika jana Kawe Dar es Salaam.
*MKUTANO WA MWAKA WA MUSACCOS WAFANYIKA DAR JANA.





Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo wa Chama cha Muhimbili Saccos, (Musaccos), Hamis Kubiga, akisoma ripoti ya mwaka wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliowajumuisha wanachama wote uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.







Wanachama wa Chama cha Mikopo cha Muhimbili Saccos (Musaccos) wakiwa kwenye Mkutano wao Mkuu wa mwaka, ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Saccos hiyo mwaka 20000, uliofanyika jijini Dar es Salaa jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.