Habari za Punde

*AFANDE AINGIZWA MJINI NA NDUGUZE, ATUMA USD 41 ZA UJENZI AJENGEWA GHOROFA YA UDONGO.

*Je ungekuwa wewe ungewafanyaje nduguzo kwa jambo kama hili??? Hili ndo Ghorofa lililogharimu USD 41,000

Wakati mwingine jamani tuwe tukifikilia na kuchanganua mambo tunapoaminiwa na ndugu, jamaa na marafiki zetu ili kujenga uaminifu na hata kujiwekea akiba ya siku ya mwisho kwa Sir God, hebu angalia nyumba hii je kweli inaweza kuwa ni ya gharama ya Dola za Kimarekani USD 41,000, kwweli bila aibu nduguyo anasota huko Duniani katika nchi za watu, anapofanikiwa kupata angalau vijisenti kidogo anawaamini nduguze na kuwatumia fedha ili kumuandalia angalau pa kufikia pindi atakapoachana na mihangaiko, na kutokana na kiasi kikubwa cha fedha anachotuma huwa na matarajio makubwa kwamba siku atakaporejea atakuta Bonge la Ghorofa na hata kama si ghorofa basi angalau Bonge la hekalu la maana na lililo katika madhali ya kuvutia.

Lakini hii imekuwa ni tofauti kwa mshkaji huyu Polisi Adivisor raia wa Uganda, ambaye ni miongoni mwa maafande walio mstari wa mbele katika kulinda Amani huko Darful, aliyejinyima na kuamua kutuma fedha zake kwa nduguze ili wamsimamie katika ujenzi, matokeo yake ndugu wakakusaidia kusimamia mjengo wa namna hii kwa gharama kubwa uliyotuma.

Haya ndo mambo yaliyomkuta police advisor wa Uganda aliyetarajia kuwa polisi wa kwanza kujenga gorofa huko nchini kwao Uganda kwa Total cost USD 41,000.

Je huu ni uungwana kweli?????????

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.