*Nyumbani kwa bosi wa wa NSSF
Hii ndiyo Nyumba ya Bosi wa NSSF, pamoja na kuwa na ulinzi mkali na nyaya za umeme zinazozuia wezi lakini bado, majambazi wameweza kutoboa tundu kweny ukuta na kufanikiwa kuingia ndani na kubeba makasha hayo ya kuhifadhia fedha na kutokomea nayo. Nyumba hiyo inavyoonekana kwa nje ikiwa na ukuta imara.
Hili ndilo tundu lililotobolewa na majambazi hayo na kukamilisha kazi yao kiulaiiiiiiniiiiiii.
Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar es Salaam
KUNDI la majambazi yasiyojulikana usiku wa kuamkia jana limevamia nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau, na kupora kasha la fedha linalodaiwa kuwa na mamilioni ambayo thamani yake haijafahamika bado.
Tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, lilitokea usiku wa kuamkia jana kwenye nyumba hiyo iliyopo Kinondoni eneo la Ada Estate.
Habari ambazo MTANZANIA Jumapili imezipata kutoka eneo la tukio, zinasema lilitokea usiku wa manane ambapo majambazi hao waliingia baada ya kutoboa ukuta wa uzio na kisha kuwateka walinzi.
Baada ya kufanikiwa kufanya hivyo, waliwalazimisha walinzi kutoa funguo za geti, wakalifungua na kuingiza gari lao ndani.
Inadaiwa baada ya hapo walifungua milango ya nyumba na kuanza kupekua vyumbani hadi katika chumba cha Dau walikolikuta kasha hilo, waliloondoka nalo pamoja na nyaraka kadhaa zilizokuwamo.
Hata hivyo wakati tukio hilo linatokea, Dau na familia yake hawakuwamo nyumbani humo.
Kwa mujibu wa majirani, majambazi hao wasiyopungua kumi yalifanikisha uvamizi wao licha ya nyumba hiyo kuwa na mfumo wa kisasa wa usalama, uliozungushwa katika uzio wote.
Habari nyingine za majirani zinasema ndani ya nyumba kulikuwamo na kijana mmoja, ambaye alifungwa kamba na kuzibwa mdomo kwa plasta huku akilazimishwa kuonyesha zilipo fedha na nyaraka walizokuwa wakihitaji majambazi hao.
Taarifa ya Kamanda Kalinga kuhusiana na tukio hilo inasema Polisi inawashikilia walinzi wawili kwa ajili ya upelelezi kamili.
“Katika hali ya kawaida haiwezekani wawe na silaha halafu watu watoboe ukuta waingie ndani bila ya kudhibitiwa,” alisema Kamanda Kalinga.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Deus Mtatilo (52) mkazi wa Kinondoni na Yusuph Bakari (56) mkazi wa Ubungo. Walinzi hao ni waajiriwa na NSSF.
“Dau na familia yake hawakuwapo, walinzi walikutwa wamefungwa kamba…katika matukio ya uhalifu kama huu zinaweza kufanyika hadaa vilevile,” alisema.
Dau mwenyewe hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo.

No comments:
Post a Comment