Habari za Punde

*MVUA ZA HAPA NA PALE DAR, MSASANI HAKUPITIKI

hii ndiyo ramani ya nyumba zinazojengwa maeneo haya ambapo hata choo huweza kujengwa dirishani kwa jirani, na inapofikia kipindi hiki cha mvua huwa ni balaa kwani maji hukosa njia ya kupita.

Huu ndiyo mtindo wa nyumba za maeneo hayo ambazo huwa Under Ggound huku zikiwa ni sehemu ya kutupia takataka.


CHOO CHA PASPOT SIZE

Hiki ni choo cha Paspot Size, ambacho ni miongoni mwa vyoo vinavyotumiwa na wakazi wengi wa maeneo hayo, ambacho huwa karaa kipindi hiki cha mvua kwani hutililisha maji machafu.


Takataka na chupa za maji zikiwa zimejaa kwenye mfereji wa kupitishia maji katika daraja la Msasani Chama na kusababisha kuziba kwa mfereji huo hali inayosababisha mafuriko katika eneo hilo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Nguzo za zege zikijengwa katika daraja la TMJ Msasani ili kuzuia magari yanayoweza kutumbukia darajani hapo kutokana na ufinyu wa barabara hiyo, ambayo hujaa maji kipindi hiki cha mvua na kutoonekana mwanzo na mwisho wa daraja hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.