Na Sufianimafoto Reporter, jijini
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri, amerejea nchini jana akitokea nyumbani kwao Zambia, tayari kuikabili timu ya Haras El Hodood katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, unaotarajiwa kufanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza jana mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Phiri alisema kuwa amekuja kuungana na timu yake kwa ajili ya kuiongoza katika pambano hilo gumu dhidi ya Haras El Hodood.
Alisema kuwa alipokuwa nchini kwao, mambo mengi yalisemwa juu yake, lakini ukweli ni kwamba bado ni kocha wa Simba na amerejea tayari kwa ajili ya kuifundisha timu yake hiyo katika mchezo dhidi ya Waarabu hao.
Alisema kuwa jana alishindwa kwenda Morogoro kuungana na timu yake kwa kuhofu kuchelewa, lakini leo anatarajia kujiunga na timu yake kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Haras El Hodood.
Alisema kuwa amefurahishwa sana na timu yake kuifunga Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ambako Simba ilishinda mabao 4-3.
“Nimefurahi sana timu yangu kuifunga Yanga, kilichonifurahisha zaidi ni maagizo yangu ya kiufundi niliyoyaacha yamefanyiwa kazi,” alisema Phiri.
Awali vyombo vya habari hapa nchini viliripoti kuwa kocha huyo amekwenda kwao kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) kwa ajili ya kuifundisha timu ya Taifa ya nchini hiyo, Chipolopolo.
Taarifa hizo za Phiri kupewa Chipolopolo ziliripotiwa siku ya nne baada ya yeye kuondoka nchini. Uongozi wa Simba ulikiri kocha huyo kuwa na mazungumzo na FAZ, ingawa walisema asingeweza kusaini mkataba na timu hiyo kabla ya kuzungumza nao (Simba).
IGP WAMBURA AWAHAKIKISHIA WANANCHI HALI YA USALAMA KUELEKEA UCHAGUZI WA
SERIKALI ZA MITAA
-
NOVEMBA 15,2024 KIDATU, MOROGORO
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amewakumbusha wananchi
kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kushiriki ...
52 minutes ago
No comments:
Post a Comment