Habari za Punde

*VURUGU ZAENDELEA UCHAGUZI SIMBA, WENGI WAKATIWA RUFAA

Na Sufianimafoto Reporter, jijini

KATIKA kile kinachoweza kutafsiriwa kama vurugu, ni wagombea wawili tu kati ya wale wanaowania nafasi za juu za uongozi katika klabu ya Simba ambao hawajakatiwa rufaa.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Frederick Mwakalebela, alisema jana kwamba wagombea watano walikuwa wamekatiwa rufani kupinga kuwa nia nafasi za Mwenyekiti na Makamu wake.
Wagombea waliokuwa wamepitishwa kuwania uenyekiti, baada ya Hassan Dalali kuondolewa walikuwa ni Mohammed Nyagomwa ‘Nanyali’, Ismail Rage, Michael Wambura, Andrew Ditta, Zakaria Hans pope na Hassan Hasanoo.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, waliopitishwa walikuwa ni Mwina Kaduguda na Godfrey Nyange ‘Kaburu’.
Mwakalebela alisema kuwa wagombea kwa nafasi ya uenyekiti ambaye hakukatiwa rufaa ni Hassan Hassano wakati waliosalia wote wamekatiwa rufaa.
Mwina Kaduguda naye naye amekatiwa rufaa katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
“Wote kwa kweli wamekatiwa rufaa wagombea hao wawili tu wa nafasi hizo za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti,” alisema.
Katika nafasi ya ujumbe, waliopitishwa kugombea ni Said Pamba, Suleimani Zakazaka, Swedy Fikirini, Khamis Ramadhani, Boniface Wambura, Vitus John, Yasin Said, Francis John na Hassani Mnyenye.
Wengine ni Hassan Mtenga, Joseph Hangare, Ibrahim Masoud, Damian Manembe, Chano Almas, Maulid Said na Bundala Benedict.










.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.