Na Sufianimafoto Reporter, Morogoro
MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Simba, jana waliweka rekodi ya aina yake, baada ya kucheza mechi 22 za Ligi Kuu bila kupoteza, baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar ya Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, mshambuliaji wake tegemeo, Mussa Hassan Mgosi, naye alijitokeza kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mara mbili na kumfanya afikishe mabao 18 msimu huu, akiwaacha wapinzani wake wa karibu, Mrisho Ngassa na John Boko.
Kwa kufunga mabao hayo, Mgosi amefikia idadi iliyofikiwa na mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Boniface Ambani wa Yanga.
Katika mchezo huo, Mgosi alifunga bao la kwanza kwa Simba katika dakika ya 15 kwa shuti kali.
Mchezaji wa zamani wa Simba, Yahya Akilimali, ambaye sasa yupo Mtibwa, alipiga shuti kali katika dakika ya 18, lakini likapanguliwa na mlinda mlango Juma Kaseja.
Na Zuberi Katwila naye nusura afunge dakika mbili baadaye, baada ya kupiga kona ya moja kwa moja lakini Kaseja tena akafanya kazi kubwa kuipangua.
Dakika tano baadaye, Mohamed Kijuso alipiga krosi iliyopanguliwa na Kado.
Dakika ya 34, Mike Barasa aliambaa na mpira upande wa kushoto na kupiga krosi
Kiungo Jerry Santo, akiwa katika nafasi nzuri alishindwa kufunga bao, kufuatia kona ya Redondo katika dakika ya 41.
Dakika moja kabla ya mapumziko, Shaaban Kado alitoka baada ya kuumia kwa mara nyingine na nafasi yake kuchukuliwa na Sudi Slim.
Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana na katika dakika ya 53, Masoud Ally aliwashangaza mashabiki uwanjani baada ya kukosa bao, akiwa yeye na nyavu baada ya Kaseja kuwa ameshatoka langoni.
Ramadhan Chombo aliipatia Simba bao la tatu baada ya kumalizia gonga nzuri katika dakika ya 57.
George Owino alitoka katika dakika ya 62 na nafasi yake kuchukuliwa na David Naftali. Na kiungo Jabir Aziz aliingia katika dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Mike Barasa.
Dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, Mussa Hassan Mgosi, aliipatia Simba bao la nne kwa kufunga kwa kichwa, kufuatia kazi nzuri ya Jabir Aziz, aliyepiga krosi
Dakika ya 89, Mwamuzi David Paul kutoka Mtwara alimpa kadi nyekundu Godfrey Magoli kwa kumuangusha Kevin Yondani.
Timu zilikuwa Simba: Juma Kaseja, Ramadhan Haruna, Salum Kanoni, Juma Nyoso, George Owino/David Naftali, Jerry Santo, Amri Kiemba, Ramadhan Chombo, Mussa Hassan Mgosi, Mohamed Kijuso, Mike Barasa.
Mtibwa: Shaaban Kado, Obadia Munyasa, Zuberi Katwila, Chacha Marwa, Dickson Daud, Shaaban Nditi, Mkopi, Masoud Ally, Omary Matuta, Monja Liseki, Akilimali Yahya.
Mjini Mbeya, mabingwa wa msimu uliopita, Yanga, walilazimika kucheza kwa nguvu kusawazisha bao la Sospeter Wega, alilofunga dakika ya 70 kwa Prison, baada ya mchezaji wake wa kimataifa wa
Na Yanga, ilimaliza msimu
Mjini Songea, Moro United ambao wameshaaga Ligi Kuu, walisimama kidete na kushuka kwa heshima, baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji, mabao hayo yakifungwa na Stephen Mwasika kwa penati dakika ya 5 na Oscar Joshua katika dakika ya 63. Said Kokoo alifunga bao la tatu dakika ya 78.
Katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Manyema walijikuta wakishindwa kupata ujanja wa kuifunga Azam, baada ya kujikuta wakimaliza kwa suluhu ya 0-0.
Jijini Mwanza, Toto, waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani, baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa matokeo hayo, timu tatu zimeteremka daraja ambazo ni Moro United, Manyema na Prison ya Mbeya.
No comments:
Post a Comment