Habari za Punde

*HIZI SIMU JAMANI, JAMAA ALIPULIWA NA SIMU KAMA BOMU



Simu hiyo ikiwa kitandani baada ya kulipuka na kuunguza godoro.

Mkono wa jamaa huyo aliyelipuliawa na simu unavyoonekana baada ya tukio hilo.

Watu wengi wamekuwa wakichaji simu zao nyakati za usiku baada ya kumaliza mihangaiko yao kuwa kuamini kuwa simu hiyo itachaji na kujaa bila bugudha, nah ii imekuwa ikifanywa na waliowengi nyakati za usiku, lakini pia hata tunapokuwa tunaendeesha magari, tunatumia ‘plagi’ zetu kwenye chaja cha magari tunayoendesha hii ni hatari.
Kwa tukio hili lililotokea siku chache zilizopita, mtu mmoja alikuwa akichaji simu ya mkononi nyumbani kwake. Simu yake ikaita na akapokea ikiwa bado ipo kwenye chaji, na kilichotokea ni kulipuka simu hiyo na kusababisha ajali ya moto uliounguza godoro wakati akiwa kitandani.
Akielezea tukio hili lililomkuta alisema kuwa “Nimefanya hivyo mara nyingi, lakini kwa hili lililonitokeanya sidhani kama nitafanya hivyo tena” alisema
Aliendelea kwa kusema kuwa, wakati akichaji simu hiyo ghafla umeme ulikatika na sekunde chache baadaye, umeme uliwaka lakini ulikuja kwa kasi na mtu huyo kupigwa ‘shoti’ na kutupwa chini. Wakati akiongea simu hiyo ikiwa kwenye chaji, kama unavyoona kwenye picha, simu imeripuka na kuunguza godoro.Wazazi wake walikimbilia chumbani na kumkuta mtoto wao akiwa hoi sakafuni, akipumua kwa shida na vidole vyake vimeungua vibaya.
Walimkimbiza hospitali, lakini alidhaniwa kama amefariki, kumbe alikuwa amezirai tu. Jamani hizi Simu ndizo tunazotumia katika maisha yetu ya kisasa tujihadhali.
Hata hivyo, yatupasa tuwe makini kwasababu kinaweza kuwa kifaa cha kuondoa uhai wetu.Kamwe tusitumie simu wakati zikiwa kwenye chaji! Kama unachaji simu na kisha ikaita, ni vyema ukaitoa kwenye waya wa chaji kwanza kabla ya kuanza mazungumzo.WATUMIE UJUMBEE WATU WENGINE WALIOMUHIMU KWENYE MAISHA YAKO!!!! Iwe wana simu au hawana. Wanaweza kuwaeleza watu wengine namna ya kufanya......



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.