Habari za Punde

*IKULI DAR ES SALAAM, YAADHIMISHA MIAKA 46 YA MUUNGANO

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Balozi wa Japan nchini, Hilosh Nakagawa, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam jana usiku iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais mstaafu wa awamu ya pili (kulia), Ali Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, wakati wa hafla hiyo Ikulu Dar es Salaam jana.

Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Lindo kutoka mkoani Dodoma kilichotumbuiza wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana usiku ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza jambo na mmoja aliyeshuhudia na kuchanga udongo wakati wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Hadija Abass Rashid. Katikati ni Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam jana usiku kuadhimisha miaka 46 ya muungano wa Tanaganyika na Zanzinbar.

Rasi Jakaya Kikwete akifurahia jambo na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam jana usiku iliyoandalia maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.