Habari za Punde

*MATUKIO MBALIMBALI YA JIJINI DAR KATIKA PICHA LEO

*“JAMANI KUMBE HII NI KAZI NGUMU EEH!, AU NDIYO KUAMKA MAPEMA KUWAHI WATEJA?” Mdada auchapa usingizi kweupeee atamsajili nani usingizini? tiGOMfanyabiashara wa Vocha, ambaye pia anafanya kazi za kusajiri laini za simu katika kituo cha daladala cha Ilala Boma Dar es Salaam, ambaye jina lake halikuweza kufahamika, akiuchapa usingizi kwenye kibanda chake wakati akisubiri wateja leo.
*“KAZI NI KAZI HAINA USISTER DUH WALA UBROTHER MEN, ZaiN
Unapokuwa katika kazi hii lazima uwe macho na makini namna hii, hivi ndivyo anavyoonekana kusema binti huyu aliyejitambulisha kwa jina la Alyce, akiwa katika kazi yake ya kusajili laini za simu za mkononi za mtandao wa Zain katika Mtaa wa Azikiwe Dar es Salaam leo, wakati akiendelea na zoezi hilo linalotegemea kukamilika mwezi june mwaka huu.

*“UBABE MWINGINE HAUFAI KAMA KIDUME HUNA NJIA YA KUJIPATIA RIZIKI MJINI BORA UBAKI HOME UTUMWE NYANYA”
Wakati mwingine unapokuwa abiria kwenye daladala fulani tena ukiwa na haraka kuwahi mahala fulani, alafu anatokea jamaa akasimama katikati ya barabara au kusababisha foleni ya kizembe nadhani ukiwa ni wewe huwa unakereka kupita kiasi ila unakuwa huna jinsi tu, huyu jamaa eti alikuwa akilizuia gari hili linalofanya safari zake Sinza-Kariakoo kupitia Tandale eneo la Moroco Hoteli, akimtaka kondakta wa gari hilo kumlipa sh. 200 ili kuruhusu gari hilo kupita eneo hilo lililokuwa na shimo waliloziba kwa mawe huku akisimamisha magari yote yanayopita hapo yamlipe kiasi hicho cha fedha. Je kwa siku anarejea home na kiasi gani? Na je akiwasimamisha wabae kama wajeda si wanamng’oa meno akirudi home atamwambia nini mkewe?.

*MIUNDOMBINU MIBOVU JIJINI DAR NI KARAA WAKATI WA MVUA”
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, wakizibua mtaro wa maji machafu katika barabara ya Uhuru jana ili kupata njia ya kupitisha maji yanayojaa katika eneo hilo wakati huu wa mvua.

*“HII NI ADHABU AU NDIYO KUJIFUNZA UJASILIAMALI SHULENI?”
Mwanafunzi wa shule ya Msingo Boma, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiwa amebeba tenga lililokuwa na majani (takataka) katika eneo la shule hiyo haikuweza kufahamika alikokuwa akipeleka tenga hilo wakati wa muda wa masomo shuleni hapo leo mchana.

*“MIUNDOMBINU YA JIJI LA DAR NI KERO KUBWA KWA WAKAZI WAKE”
Wakazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam, wakizibua mtaro ili kuruhusu maji yaliyokuwa yametuama katika barabara ya Uhuru eneo la Buguruni Sheri leo.

*“‘OPERESHENI’ HII NI KWA WILAYA YA ILALA PEKEE?”
Askari wa Kikosi cha Zima moto cha Halmashauri ya jijini Dar es Salaam, wakisimamisha magari na kuyakagua kama lina kifaa cha kuzimia moto Fire Extinguisher katika Barabara ya Uhuru eneo la Buguruni Malapa leo. Baadhi ya madereva walilalamikia utaratibu huo na kuhoji kuwa mbona askari hao hawapo katika maeneo mengine ya jiji na kuendeleza zoezi hilo?







No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.