Rais Jakaya Kikwete akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati akiingia kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 46 ya Tanganyika na Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Rais Mtstaafu wa awamu ya tatu, Rais Mkapa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru.
Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya akikagua gwaride.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akikagua gwaride.
Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya akikagua gwaride.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akikagua gwaride.
Shambla shambla za sherehe hizo, haya si maua lah hasha ni vijana walioandaliwa wakiwa wamejipanga katikati ya uwanja na neno unaloweza kulisoma mwenyewe ndugu msomaji.
"Duh! kumbe kazi hii ngumu namna hii balaa tupu afadhali ya kushika kamera, washkaji wananipiga mapicha yaani wananilenga mimi tu"
Huyu si mwingine ni aliyekuwa mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Hassan Mdeme, akiwajibika katika paredi wakati wa sherehe hizo, akiwaacha hoi wapiga picha wenzake kwa kuonyesha ukakamavu na usiriasi kana kwamba si yule tuliyekuwa tukihaha naye katika kusaka mafoto ya kuuza magazeti.
"Nasisi tupo jamani ambao hamtujui mtuone sasa sisi ndiyo tulichanganya udongo wa Muungano jamani"
Hawa ni watu muhimu sana katika sherehe kama hizi za maadhimisho ya Muungano, na kama wangelikuwa katika nchi nyingine Duniani basi nadhani wangekuwa katika hali fulani katika nguzo za Taifa, kwani hawa ni waliochanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar wakati huo wakiwa ni vijana.
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Seif Shalif Hamad, wakati wa sherehe hizo.
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wariohudhuria katika Sherehe za kutimiza miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment