Habari za Punde

*WANAFUNZI 40 WA KIDATO CHA KWANZA 2010 WAPEWA UJAUZITO

Na Editha Karlo,Tunduru
Wanafunzi 40 kati ya 86 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule ya sekondari ya Malumba iliyo Wilayani hapa hawajaripoti kutokana na kubeba mimba huku wengine wakiwa tayari wameshajifungua. Hayo yamesemwa na Diwani wa kata ya Malumba Msenga Said wakati akiongea na Mtanzania,alisema kata yake inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupata mimba za utotoni. Alisema mwaka 2007 sekondari ya Malumba ilipokea wanafunzi wa kike wakujiunga na kidato cha kwanza wapatao 32,lakini mpaka sasa waliofanikiwa kufika hadi mwaka huu wa mwisho ni wanane tu. Mhe. Said alisema jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa hizi mimba za utotoni ni ngoma za unyago maarufu kwa jina la msondo ambazo huchezwa usiku na huchezwa msichana anayeanzia umri wa miaka saba. Alisema msichana aliyevunja ungo huambiwa kumnyima mwanaume ngono au kumuogopa ni dhambi hali ambayo huwa fanya kushiriki ngono katika umri mdogo. " kwakeli hizi ni mila potofu sana na zinachangia idadi ya mimba utotoni na kuwanyima watoto wakike haki yao ya msingi kwenda shule"alisema Said Takwimu za sekondari hiyo zinaonyesha hadi kufikia Aprili mwaka huu wanafunzi 38 kutoka madarasa tofauti wamepata mimba na kuacha masomo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.