Evelyn Mkokoi, Kagera
Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Uongozi wa Mkoa wa Kagera umetakiwa kuongeza jitihada za kutosha katika kuhahakisha kuna kuwepo na uelewa wa kutosha katika utekelezaji wa suala zima la sheria ya Mazingira.
Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkuregenzi wa Idara ya Mazingira kutoka kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bw Richard Muyungi alipokuwa katika ziara ya Ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na Mkakati wa Hifadhi ya Mazingira ya Ardhi na vyanzo vya maji katika Mkoa wa Kagera.
Bwana Muyungi ameeleza kuwa watendaji wengi wana mapungufu ya kutokufahamu na kuitumia Sheria ya Mazingira na ndo maana kumekuwa na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika Mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na ule utokanao na uvamizi wa wawafugaji kutoka nchi jirani za Rwanda na Uganda.
Bwana Muyungi ameongeza kuwa uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti kwa matumizi ya nishati ya mkaa na utengenezaji wa mbao ni mkubwa hasa katika msitu wa Biharamuo hivyo maafisa misitu, mazingira pamoja na idara ya mahakama wana kila haja ya kutumia nyezo na mamalaka walizo nazo ili kuweza kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria ya mazingira waharibifu hao.
Aidha kwa upande wake RAS wa Kagera Bi Maria Bilia, ameeleza kuwa, ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira, serikali itengeneze matuizi bora ya ardhi, ili wananchi waweze kutengewa maeneo ya ufugaji, ya kilimo, kuishi na maneo ya hifadhi yatengwe na elimu itolewe ya kutosha juu ya hifadhi ya mazingira, kwani tatizo hili ninachagiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya umaskini inayopelekea wanachi kufanya hivyo ili kujipatia kipato. Alisisitiza.
Ufuatiliaji wa utekelezaji wa shera ya mazingira na Makakati wa Hifadhi ya mazingira ya Ardhi na vyanzo vya Maji, unafanyika nchi nzima ili kuweka kukamilisha ripoti ya hali ya mazingira nchini.
Picha kwa hisni ya www.fullshangwe.blogspot.com
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 14, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam November 14,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za M...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment