Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar
MECHI ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyokuwa ichezwe keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam sasa imesogezwa mbele hadi Aprili 18 mwaka huu.
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ilikutana na viongozi wa timu zote mbili na kufikia uamuzi huo ili kujali na kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa mashabiki ikiwa ni pamoja na kuzihakikishia timu zote kuhusu haki katika mgawanyo wa mapato.
Awali timu hizo pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walikubaliana mchezo huo uchezwe katika uwanja wa Uhuru ili kukwepa gharama kubwa za makato ya kulipia uwanja huo zinazokatwa na serikali na kusababisha timu kuambulia mapato ya mlangoni kiduchu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sethi Kamuhanda, alisema kuwa makubaliano hayo yameafikiwa katika kikao cha pamoja ambapo pia wanatarajia kukutana na kujadili namna ya kuwapunguzia makato hayo.
Alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na mchezo huo kuvuta hisia za mashabiki wengi wa timu hizo ambao baadhi yao hutokea mikoani ili kushuhudia mtanange wa watani hao wa jadi, hivyo kama mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Uhuru basi watu wengi watashindwa kufika kupata burudani hiyo kwa kukwepa vurugu na msongamano.
“Tumeangalia maeneo mawili ya ulinzi na usalama pamoja na mgawanyo wa mapato, hivyo naomba radhi kwa mashabiki kwa usumbufu ambao utajitokeza lakini tumefanya hivi ili kuona watu wote wanaopenda soka wanashuhudia mchezo huo,” alisema Kamuhanda.
Naye Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema wameridhia makubaliano hayo kwa kuzingatia maeneo hayo yaliyozungumziwa.
“Tunawaomba radhi mashabiki wa Yanga waliokuja kutoka maeneo mbalimbali nchini kote” alisema Madega.
Naye Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali aliafiki makubaliano hayo kwa pende zote na serikali yaliyotolewa na Katibu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Uwanja.
SERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIONDO MBINU SUA
-
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Takribani shilingi bilioni 41 zimetolewa na serikali kupitia Mradi wa Elimu
ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment