Beki wa Simba Kelvin Yondan, akishangilia huku akiwa amevaa jezi ya Yanga baada ya mchezo huo kumalizika na wachezaji wa Yanga na Simba kubadilishana jezi.
Warembo wa Vodacom, wakipozi na Kombe wakati wakisubiri zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo ya Vovacom, ambapo Kombe hilo lilikabidhiwa kwa Simba Sports Club, mabingwa wapya wa ligi hiyo 2010.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na Kombe lao baada ya kukabidhiwa, Kombela Ubingwa wa Ligi Kuu wa Vodacom Tanzania Bara.
"Kwa upupu huu lazima wanikome si Mgosi wala Boko"
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akifanya mauza uza katika goli 'akinaniliu' kabla ya kuanza kwa mtanange huo katika ya Yanga na Simba zote za Dar es Salaam uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni Kigi Makasi.
"Wacha niatishe si wamezoea mauza uaza na mauchawi basi hapo miroho inawadunda, kuniona nainama hapa"
Kocha Mkuu wa Yanga, Papic, akiigiza kunyunyiza naniliu, huku akishangiliwa na mashabiki wa Yanga kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
"Kama umetumwa utanijua mie ni nani kafie mbali huko, kumbe ndo maana wanatuotea kizembe"
Athuman Idd 'Chuji', akimpiga teke Njiwa aliyeingia katikati ya uwanja na kuanza kuzunguka bila kuogoa huku akipishana na wachezaji na mpira, na alipokuwa akifukuzwa njiwa huyo hakuwa akiruka wala kukimbia bali alikuwa akizunguka tuuuuu, wakati mchezo ukiendelea uwanjani hapo.
Heka heka langi mwa langoni la Simba.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja, akijaribu bila mafanikio kuokoa mpira wa penati uliopigwa na Jerry Tegete, na kuandika bao la 3, goli lililomfanya Kaseja kulia kwa uchungu.
Njiwa akimpiga chenga Athuman Idd.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimtesa beki wa Simba, Kelvin Yondan, wakati wa mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 4-3.
Chuji akijandaa kupiga shuti wakati wa mchezo huo.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja, akiwa hoi langoni mwake baada ya kushindwa kuukoa mpira uliopigwa na Chuji na kuandika bao la kwanza la kusawazisha kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Pamoja na Yanga kuwa nyuma kwa kufungwa lakini bado mashabiki wake hawakuchoka kushanglia muda wote.
No comments:
Post a Comment