Habari za Punde

WAREMBO WA MISS UNIVERSE WATEMBELEA KIWANDA CHA BIA SERENGETI

Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti, Bahati Singh, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati Warembo wa Miss Universe, walipotembelea katika Ofisi hizo na Kiwanda kinachotengeneza Bia hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shindano hilo linalotarajia kufanyika keshokutwa. Katikati ni Ofisa Uhusiano mwandamizi wa SBL, Imani Lwinga na Meneja wa Bidhaa Nandi Mwiyombella.

Bahati Singh, akiendelea kutoa maelezo kwa waandishi wa habari (nyuma yake) ni warembohao wakipozi.

Warembo wakipozi wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wakati walipotembelea kiwanda hichi kilichpo Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana.

Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar es Salaam

WAREMBO wanaotarajia kushiriki katika shindano la kumtafuta Miss Universe 2010, leo wametembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti ambao ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo linalotarajia kufanyika keshokutwa jijini Dar es Salaam.
Warembo hao wamefanya ziara hiyo leo na kula chakula cha mchana pamoja na viongozi wa Kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya kujifunza kuhusiana na na kujionea jinsi Bia ya Serengeti inavyoweza kuandaliwa hadi kukamilika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) Nandi Mwinyombella, aliwaasa warembo hao kujiepusha na vishawishi na vitendo viovu vinavyoweza kuwapotezea heshima mbele ya Jamii.
“Wasichana wengi wamekuwa wakiingia kwenye vishawishi hivi kutokana na kujiingiza katika makundi ambayo hayana maana ila sisi kama SBL lengo letu la kudhamini mashindano haya ni kuendeleza vipaji vya wachichana ambao kupitia urembo baadaye wanaweza kujiajiri wenyewe, na pia tunatarajia kupata mabalozi wazuri kutoka katika shindano hili watakaoweza kuitangaza vyema kampuni yetu.” alisema, Nandi
Aidha alitaja tarehe ya shindano hilo kuwa ni Aprili 23, yatakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.