Habari za Punde

*AKUDO IMPACT YATAMBULISHA WANENGUAJI 4 WAPYA

Kiongozi wa Bendi ya Akudo Impact, Christiane Bella, akiwatambulisha wanenguaji wapya aliokuja nao kutoka Kinshasa,waliojiunga na bendi hiyo, ambao wote walikuwa katika bendi kubwa maarufu za nchini humo, alitaja bendi walizotoka kuwa katika bendi za Fally Ipupa, Bileku, Bozi Boziana na mmoja ni yule aliyewahi kuitumikia bendi hiyo siku za nyuma na kwammba sasa amerejea upya.


Francine Pesabiloko, aliyekuwa na kundi zima la Fally Ipupa, akipozi wakati wa utambulisho huo.

Fany Bosawa, aliyewahi kuwa na bendi hiyo siku za nyuma na kutimkia Kinshasa.

Patricia RG 512, aliyekuwa na kundi zima la Bileku Mpasi, akipozi.
Raissa Sangwa, aliyekuwa na kundi zima la Bozi Boziana, akipozi.

Christiane Bella, akizungumza wakati akijibu maswali kuhusiana na utambulisho huo. (kushoto) ni Meneja wa bendi hiyo, Fadhili Mfate na (Kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa bendi hiyo, Michael Andrew.

Christiane Bellah, (katikati) akipozi kwa picha na wanenguaji wake wapya.

Wanenguaji wapya wa bendi ya Akudo Impact, kutoka (kushoto) Fany Bosawa, Francine Pesabiloko, Raissa Sangwa na Patricia RG 512, wakishambulia jukwaa wakati wa utambulisho wao baada ya kujiunga na bendi hiyo wakitokea nchini Kinshasa Kongo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Stereo Kinondoni Dar es Salaam leo mchana.

Wanenguaji wapya wa bendi ya Akudo Impact, kutoka (kushoto) Fany Bosawa, Francine Pesabiloko, Raissa Sangwa na Patricia RG 512, wakishambulia jukwaa.









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.