
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza kwa makini Mkufunzi kutoka Mradi wa ‘CHAMPION’, unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Watu wa Marekani USAID, chini ya Shirika lisilo la Kiserikali EngenderHealth, Sara Teri , akiendesha mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu maambukizi ya Ukimwi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Hawa ni baadhi ya maofisa wa CHAMPION, wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock, wakifuatilia kwa makini mada liyokuwa ikiwasilishwa na mwenzao mbele.

Semina hiyoilikuwa na vitendo pia ili kuweza kufikisha ujumbe uliokamilika, kama unavyoona picha ni baadhi ya waandishi wakiwa na karatasi zilizo na majina au kazi wanazofanya watu mbalimbali, ikiwa ni mfano tuuu, huyu jamaa wa kwanza kama unavyosomakaratasi yake ikiwa imeandikwa 'CANGUDOA' inaama kwa wakati huo alikuwa akiigiza kama changudoa ambapo alitakiwa kuonyesha wateja wake miongoni mwa walio na karatasi kwa kusoma majina ambao humtembelea mara kwa mara, naye aliwateua bila kusita ambapo wateja wake walionekana kuwa wengi ni madereva taxi, Polisi, na wengineo jambo ambalo ni kweli kwani Machangudoa hutembelewa zaidi na watu hao.

Dk. Ben Ngoye, akiendelea na somo la HIV AIDS.
No comments:
Post a Comment