Habari za Punde

*KOMBAINI YA IRINGA KUMENYANA NA WANAIGERIA

TIMU ya mkoa wa Iringa, Ruaha Stars leo itapambana na timu ya kombaini ya wachezaji wanaotoka Nigeria waliokuja kutafuta timu nchini.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Uhuru, kwa mujibu wa kocha mkuu wa timu ya Ruaha Stars, Fred Felix Minziro.Minziro alisema kuwa mechi hiyo ni muhumu sana kwa timu yake kwani itawapima wachezaji wake uwezo kabla ya kuanza kwa robo fainali ya Kili Taifa Cup hapo Mei 24. Iringa itapambana na mabingwa watetezi, Ilala.
Alisema kuwa wamejinadaa vilivyo kukabiliana na timu hiyo ya Nigeria na bila shaka wataibuka na ushindi mnono. Iringa pia inaundwa na wachezaji nyota wakiongozwa na Athumani Idd ‘Chuji’, Godfrey Bonny na Salum Swed.
Alifafanua kuwa wa wachezaji hao wa Nigeria watatoa changamoto kubwa kwa wachezaji wake ambao lengo lao kubwa safari hii ni kutwaa ubingwa na kuweha historia. Alisema kuwa wanafanya mazoezi asubuhi na jioni ili kuwa kamili katika mashindano hayo.
Kwa upande wa kiongozi wa timu ya Nigeria, alisema kuwa ana wachezaji 13 aambao wamekuja nchini kwa lengo la kutafuta timu za kujiunga nazo.Wakati huo huo; mechi ya Kijitonyama Stars na Ruaha Stars iliyopangwa kufafanyika leo imehairishwa kutokana na uchovu wa mazoezi wa wachezaji wa timu ya mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.