BONDIA maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Francis “SMG” Cheka leo anashuka ulingoni nchini Uingereza kuwania mkanda wa uzito wa kati wa Jumuiya ya Madola.
Cheka atapambana na bondia Martin Murray katika pambano lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa St Helens.
Cheka alipata nafasi hiyo baada ya kuondolea katika pambano hilo, bondia Darren Barker.
Meneja wa bondia huyo, Juma Ndambile alisema jana kwa njia ya simu kutoka Sheffield, kuwa bondia wake yupo katika ari kubwa ya kutwaa ubingwa huo kutokana na maandalizi ambayo ameyafanya mpaka sasa.Ndambile alisema kuwa bondia wake amejinadaa vilivyo na yupo tayari kuweka rekodi nchini Uingereza kwa kushindwa pambano hilo na kurejea na mkanda hapa nyumbani.
“Lengo letu ni kufanya vyema na si vinginevyo, tumejiandaa sana na kama ukanvyojua, Cheka alikuwa nchini Kenya akijifua na mpaka sasa hana tatizo lolote, tunaomba watanzania watuombee dua ili kuibuka na ushindi,” alisema Ndambile.Alisema kuwa Cheka hajawahi kushinda nchini Uingereza nah ii ndiyo nafasi yake kubwa kufanya vyema na kuweka historia mpya.
Cheka mpaka sasa anashikilia mataji mawili ya uzito wakati wa vyama vya UBO na ICB.“Nimejiandaa vyema, nataka kufuta aibu kwa mabondia wa Tanzania kushindwa kutamba nje ya mipaka yetu, nipo fiti kukabiliana na mpinzani wangu ambaye ana rekodi nzuri,” alisema Cheka.
DKT. NCHIMBI AWANADI WAGOMBEA UBUNGE, MADIWANI WA SIMIYU KWA WANANCHI
-
MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM),Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na wananchi
alipokuwa aki...
46 minutes ago
No comments:
Post a Comment