Habari za Punde

*BASI LA SAMMA LAJERUHI 29 WILAYANI GEITA

Na Victor Bariety, Geita

WATU 29 wemejeruhiwa vibaya huku wanne kati yao hali zao ni mbaya wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kufuatia ajali iliyolihusisha basi la kampuni ya SAMMA lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Kigoma katika kijiji Mpovu katika wilaya ya Geita mkoani mwanza .
Kwa mujibu wa jeshi la polisi mkoani Mwanza zilizothibitishwa na kamanda wa mkoa Simoni Sirro ni kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 3.30 asubuhi leo baada ya Basi hilo lenye namba za usajili T236AAN aina ya ISUZU lililokuwa likiendeshwa na Siasa Benard kuligonga Lori lenye namba T170AUA ambapo dereva wake hakuweza kutambuliwa mara moja lililokuwa likiingia katika barabara kuu bila tahadhari.
Taarifa kutoka jeshi la polisi zimeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Dreva wa Lori kushindwa kuingia katika barabara kuu kwa uangalifu na hivyo kusababisha basi kuligonga lori kwa mbele na kuanguka na kusababisha majeruhi 30 na 4 kati yao hali zao ni mbaya.
Akithibitisha kupokea majeruhi hao Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya Dr.Omari Dihengo amewataja majeruhi hao kuwa ni Msilo Mwita [20],Amosi Mita[31],Faraja Kagasheku[31],Joyce Charles[40],Salima Daudi [54],Suzana Bakamola[28] wote wakazi w Mwana wengine ni Legesa John[21],Nifa Sia[35], Inocenti Kabiligi[20],Mibulo Fiakero[34],Issa Emed[28],Emmanueli Mathias[25] wote wakazi a wilayani Ngara mkoani Kagera
Wengine ni Kaego Uria(25)mkazi wa nyakanga,Charles Mayala(24),Osard Kaloli(21)Mkazi wa Kibondo,Elizabert Paulo(20 mkazi wa Chato,Meresiana Nyilila(35)na mwanae Shija mhangwa(4)wakazi wa Chato.
Wengine waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Kipara Lusamu(28)mkazi wa geita,Kulwa Elias(20)mkazi wa nyamikoma, Erasto Emiry(50)mkazi wa Mwanza pamoja na josephine Faustine(14)mkazi wa sengerma.
Kwa mujibu wa mganga huyo hali za majeruhi wanne kati yao ni mbaya na kwamba wanafanya utaratibu wa kuwapeleka katika hospitali ya lufaa ya bugando jijini mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao hali iliyopelekea kupoteza fahamu.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Erasto Emiry ambaye amevunjika mkono wa kulia,Emanuel Matias ambaye ameumia sehemu za kifuani,Meresiana Nyilila aliyeumia mwili mzima na Mbusilo mwita ambaye alifikishwa hospitalini hapo akiwa hana fahamu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.