"Hapa hatuondoki ng'ooo, hadi tuone akipanda karandinga, au vipi Mjwahuzi?"
Baadhi ya wapiga picha za habari wa magazeti mbalimbali, wakiwa nje ya geti nyuma ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakisubiri kumuona Liyumba akipanda katika gari la wafungwa kuelekea jela, baada ya kuhukumiwa.
"Duh! yaani siamini macho yangu ndo nakwenda jela hivi hiviiii, "

Amatus Liyumba, akijifuta jasho lililokuwa likimtililika kwa waingi baada ya kusomewa shitaka lake na kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana.

Mtuhumiwa wa kesi ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi, Amatus Liyumba, akiwa chiniya ulinzi wakati akisindikizwa kuingia ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana kutolewa hukumu ya kesi yake, ambapo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Liyumba, akisindikizwa na askari chini ya ulinzi mkali kutoa katika sero za mahabusu kuingia Mahakamani.

Liyumba akizungumza na wakali wake baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa muda kabla ya kutolewa hukumu.

Mama huyu alionekana kuwa bize muda wote mahakamani hapo, akienda huku na huko na kurudi, hapa alikuwa akitoka chumba cha Mahabusu, imeelezwa kuwa mama huyu ni mmoja kati ya wale wenye uhusiano na Mtuhumiwa huyo Liyumba.

MAhakamani hapo hata machizi pia walikuwapo, hebu mcheki jamaa huyu, sijui alikuwa akimahanisha nini, Eti alibana kwenye kona mlangoni akimsubiri Liyumba ili aonekane kwenye Kamera za mapaparazi, tena eti kwa mapozi kama haya utazani yupo katika jukwaa la muziki wa Bongo Flava.

Hapa ni wakati akirejea kwa mara ya pili kwenye chumba cha mahakama, baya kuahirishwa kwa kesi hiyo kwa muda.

Hizi ndizo zilikuwa pozi zake za mwisho mahakamani hapo kabla ya kuhukumiwa. huku jasho lukuki likimtililika.

Wakati akisubiri kuhukumiwa mahakamani hapo.

Liyumba (katikati) akizungumza na mawakili wa Serikali na Wakili wake (kushoto) wakimfafanulia juu ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment