Habari za Punde

*NANI KUNUNA, NANI KUCHEKA LEO, MAN U AU CHELSEA?

Mashabiki wa timu ya Manchester United ya Uingereza, wakiwa na furaha wakati wakifuatilia mchezo wa timu hiyo na Sunderland katika ukumbi wa Slip Way. Katika mchezo huo Man U ilifikisha jumla ya Point 82 na kupishana ponti 1 na Chelsea na kuwaacha mashabiki hao wakisubiri mechi za leo ambapo timu zote zinacheza, Iwapo Man U ikishinda na Chelsea ikapoteza mchezo basi Bingwa wa ligi hiyo atakuwa ni Man U kwa mara ya nne mfululizo.

Hawa ni watoto Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Frederick Mwakalebela, ambao ni mashabiki wakubwa wa chama la Chelsea, ambo huwa wanashindwa kwenda shule ama kula chakula pindi chama lao linapopoteza mchezo yaani kufungwa, watoto hawa walipiga picha hii ya kumbukumbu, siku ya mchezo wa Chelsea na Liverpool, ambapo Chelsea ilifikisha jumla ya Point 83 wakiwa mbele kwa point moja dhidi ya wapinzani wao Man U. Je watoto hawa leo jioni watashindwa kula chakula ama watakula kwa furaha zote?


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.