Habari za Punde

*SOFIA SIMBA ALIA NA PROPAGANDA ZA MATANGAZO

NaEliya Mbonea, Arusha
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Sofia Simba
amewataka wanawake nchini kuachana na propaganda za
matangazo yanayoikosoa Serikali na Ilani ya Uchaguzi ya CCM.Simba ambaye pia ni Waziri wa Utawala Bora aliyasema hayo juzi
mjini hapa wakati akizungumza na wanawake wa mjini Arusha
ikiwa ni muendelezo wa ziara yakemkoani hapa.“Wanawake msikubali mchanganywe na matangazo
yanayodai ‘sidanganyiki’ hao endeleeni kuwapuuza na kamawao
wakisema hivyo sisi tuseme “hatubabaishwi,” alisema Simba.Katika kusisitiza kauli yake Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba,
wanawake wanapaswa kuendelea kutumia kauli ya kauli mbiu
isemayo hatubabaishwi ili kujiepusha na maneno yakizushi yanayotolewa dhidi ya Serikali ya Rais Kikwete.Alisema wanawake wanapaswa kuyapuuza maneno hayo kwa kiasi
kikubwa kwani yamekuwa yakitolewa na viongozi wa upinzani
hususani wanapobeza maendeleo yanayofanywana Serikali ya CCM. Aliwataka viongozi wa jumuiya hiyo na hata wale wa chama
kuyafuta maneno hayo ya kizushi mara tu yanapotolewa kwa
kuitisha mikutano ya hadhara na kujibu hoja hizo badala ya
kuziacha ziendelee kuwaumiza vichwa wanachama na hata
wananchi kwa kudhani yana ukweli.Katika hatua nyingine Simba aliwataka wanawake kuacha
kuendekeza ubinafsi, majungu, masuala ya udini na uakabila
badala yake wajielekeze katika kutambua kwamba wao ni watotowa baba na mama mmoja ambaye ni CCM. “Tukiwezakuifuta hali hii hakika itatufikisha mbali sisi wanachama na
watanzania kwa ujumla,”alisema Simba.Mwenyekiti huyo wa (UWT) Taifa alikuwa mkoani Arusha kwa siku
tatu kukagua shughuli za maendeleo Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja
na kuhamasisha mambo mbalimbali yakiwamo ya kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.