Habari za Punde

*WABANGLADESH 18, WAKAMATWA MBAGALA

watuhumiwa wa kesi ya kuishi nchini bila kibali, Raia wa Bangladesh 18, waliokamatwa Mbagala jijini Dar es Salaam Mei 16 mwaka huu wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisuru leo, wakusubiri kusomewa shitaka lao. Watuhumiwa hao walikamatwa wakati wakijiandaa kuondoka nchini kuelekea Kusini mwa Afrika, ambapo wenyeji wao ambao ni raia wa Tanzania, Daniel Kandulu na Salum Kitumbalio, waliokuwa wakiwatoza dola 200 kwa siku kwa kila mmoja wa watuhumiwa hao, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jera baada ya kukili kutenda kosa hilo la kuwahifdhi Wabangladeshi hao nchini kinyume na sheria. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 7 mwaka huu itakapotajwa tena.

Baadhi yao, wakimsikiliza kwa makini mkalimani wao kabla ya kunza kusikilizwa kesi hiyo.

Wengine wakijificha sura zao ili zisinaswe na kamera ya Sufianimafoto.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.