Habari za Punde

*FM ACADEMIA KUPAMBA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE 2010

Mratibu wa shindano la Miss Chang'ombe 2010, Tom Chilala(wapili kulia waliokaa) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitangaza burudani zitakazopamba shindano lake linalotarajia kufanyika siku ya Ijumaa, Juni 4 mwaka huu kwenye ukumbi wa TCC Chang'ombe jijini. Tom alisema kuwa katika onyesho hilo kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi mahiri ya Fm Academia Wazee wa Ngwasuma pamona kikundi cha Sanaa cha Machozi kutoka Temeka. Aidha aliwataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni pamoja na Vodacom, Redd's, Overmeer Cellars, Taafif na Tesco Faniture, ambapo kiingili kitakuwa ni Shilingi Elfu kumi tu 10,000 kwa watu wote.

Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Distillers Lmt, Martha Bangu (katikati) akielezea udhamini wa kampuni yake na jinsi walivyojiandaa kuhakikisha shindano hilo linakwenda kama lilivyopangwa. Kushoto ni mwalimu wa warembo hao, Vumilia Wilbroad (kulia) ni Tom Chilala.

Warembo hao wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.

Tom Chilala akizungumza mbele ya waandishi wa habari.

Baadhi ya warembo wakipozi.......





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.