Habari za Punde

*MADEGA, KAWAMBWA WAREJESHA FOMU BAGAMOYO LEO

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Imani madega (katikati) akisindikizwa na wanachama wa CCM na wapambe wake wakati akiingia kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Bagamoyo leo mchana kurudisha Fomu za kuomba kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama hicho.

Imani madega akiwa na familia yake ambao ni miongoni mwa watu waliomsindikiza kurejesha fomu hizo leo, (katikati) ni mtoto wake wa kwanza, Rahma Madega na mkewe, Mwanakesy Madega, pamoja na baadhi ya wapambe wake.

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Imani Madega, akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo, Katibu wa Ofisi ya CCM wa Wialaya ya Bagamoyo, Fikirini Masokola, wakati akirejesha fomu hiyo leo mchana mjini Bagamoyo.

*SHUKURU KAWAMBWA NAYE AREJESHA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA BAGAMOYO.
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Bagamoyo kwa tiketi ya CCM, Dk. Shukuru Kawambwa, akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo, Katibu wa Ofisi ya CCM wa Wialaya ya Bagamoyo, Fikirini Masokola, wakati akirejesha fomu hiyo leo mchana.

*DUNDUMA NAYE KUCHUANA NA MADEGA CHALINZE
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Nasoro Dunduma, akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo, Katibu wa Ofisi ya CCM wa Wialaya ya Bagamoyo, Fikirini Masokola, wakati akirejesha fomu hiyo leo mchana.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.