Habari za Punde

*JANUARY MAKAMBA AKUBALIKA KAMA 'OBAMA' BUMBULI










MGOMBEA Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimbo la Bumbuli, Januari Makamba, jana alipokewa na kusindikizwa na wanachana na wapambe wake kwa mbwembwe kwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.





January aliyeongozana na mama na dada yake pamoja na baadhi ya wanafamilia alitikisa mji huo wakati alipokuwa akipita katika mitaa ya mji huo kuelekea Ofisi za CCM za Wialaya ya Lushoto.

Wanachama hao Lukuki walijipanga pembezoni mwa barabara huku wakipiga ngoma kuimba na kucheza na wengine wakizuia msafara huo ili kumta mgombea huyo kushuka ili kuwasalimia kabla ya kuendelea na safari yake.


Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Makamba alipongeza taratibu za uchaguzi wa mwaka huu unaotoa nafasi kwa wanachama wote kupiga kura za maoni tofauti na ilivyokuwa awali na kuwataka makada wa chama hicho kufuata taratibu na misingi katika kuchagua wawakilishi wao.

“Leo ni siku niliyoisubiri sana baada ya kuweka dhamira ya kuwaongoza wananchi wa Bumbuli, sasa nimeirasimisha siku hii… nawashukuru wapiganaji wangu wote. Unajua siasa ina maneno na vigingi, lakini walinipa moyo na hatimaye tunaanza mchakato.

“…Napenda kuwaomba wote wanaoniunga mkono, ndani na nje ya jimbo letu la uchaguzi, kuufanya mchakato huu kwa misingi na utaratibu wa chama chetu,” alisema Makamba aliyeongozana na msafara wa mamia ya wapigakura wa Bumbuli waliokuwa kwenye magari na pikipiki.

Hata hivyo, kabla ya kuchukua fomu hizo kada wa chama hicho, Shaban Omary Bosnia , alijitolea sh 500,000 kwa ajili ya kuchangia gharama za uchaguzi za Chama hicho, akiamini kuwa ni kijana pekee mwenye dhamira na maono ya kuibadili Bumbuli kimaendeleo.

Makamba alichukua fomu hizo jana kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Lushoto, Loth Olemeirut, kisha kujaza na kurejesha huku akisindikizwa kwa karibu na mama yake mzazi.

Mpaka jana, jumla ya wagombea watatu wa ubunge katika jimbo la Bumbuli, walijitokeza kuchukua fomu. Wagombea hao ni Abdulkadir Kaniki na Abubakar Mshihiri huku mbunge anayemaliza muda wake, William Shellukindo akitangaza kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha nne.






















No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.