*Marafiki wa karibu wazimia na kupoteza fahamu....
Rafiki wa karibu na marehemu Primtiva Pancras, Rachel Mrisho akishindwa kuvumilia baada ya kuona sura ya mwisho ya marehemu rafiki yake kipenzi, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu kabla ya kupelekwa kuzikwa kwenye makaburi ya Kisutu Kinondoni leo mchana. Rachel ni mmoja kati ya marafiki wa karibu wa marehemu, ambaye alizimia na kupoteza fahamu na kupelekwa Hospitali ya Dk. Mvungi Kinondoni kwa ajili ya kupatiwa matibabu na huduma ya kwanza, wakati wa ibada hiyo iliyokuwa sambamba na kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye Kanisa la Roma Hananasifu Kinondoni.
Kimataifa : Rais Samia Aondoka Kuelekea Urusi kwa Ziara ya Kitaifa
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nye...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment