Habari za Punde

*tiGO YAKABIDHI ZAWADI ZA PROMOSHENI YA MAISHA, JIKOKI NA TIGO

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando, akimkabidhi funguo ya Pikipiki aina ya Bajaji, mshindi wa Promosheni ya 'Maisha na Tigo' Bi Aisha Sheyo. Kulia ni Kaka wa Aisha, Gerald Sheyo. Kwamawasiliano zaidi kuhusiana na ufafanuzi wa Promosheni na jinsi zinavyotolewa zawadi za promosheni hizi zinazoendeshwa na Mtandao wa Tigo, piga namba 0713 123 727 , kwani promosheni hizo zimeongezewa muda ili kuwawezesha wateja wengi wa mtandao huo kunufaika ambapo sasa mshindi atajinyakulia kitita cha Sh. milioni 100 napi kumbuka bado kunashindano la sajili na ushinde ambalo linaweza kukupatia nyumba ya kifahari wewe mteja wa tiGO.

Aisha Sheyo, mkazi wa Kiwalani Jijini Dar es Salaam, akifurahia zawadi ya pikipiki aina ya Bajaji baada ya kukabidhiwa na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Jacskon Mmbando (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Promosheni ya ‘Furahia Maisha’ inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Jackson Mmbando, akimkabidhi zawadi ya Laptop ndogo na Simu aina ya Brack Berry, mshindi wa Promosheni ya 'JIKOKI' Hellen Mbise, mkazi wa Buguruni Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Promosheni hiyo, iliyofanyika leo mchana. Katikati ni Ofisa Viwango wa Tigo, David Zacharia.

Ofisa Viwango wa Tigo, David Zacharia , akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh milioni 2, mshindi wa promosheni ya Jikoki na Tigo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za Tigo Jijini dar es Salaam leo mchana.

Na Mwandishi Wetu, Jijini
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, jana imekabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Jikoki na Tigo ambayo inaendelea kwa miezi miwili sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano hayo, Ofisa Habari wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando alisema kuwa promosheni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa wateja.

“Leo tunawakabidhi washindi wetu wiki hii, lakini promosheni hii ni maalum na ni rahisi kushinda na kujipatia zawadi”, alisema.

Alisema kuwa mteja anatakiwa kutuma neno Jikoki kwenda namba 15010 ili kushiriki promosheni hiyo.

“Kila ujumbe anaotuma atapata pointi zinazohesabika kwenye ushindi, baada ya hapo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mara nyingiili kujiongezea pointi nyingi za kushinda”, alisema.

Alisema kuwa gharama ya kila ujumbe wa promosheni hiyo ambayo itamalizika Agosti 22 ni Sh 360.

Alisema kuwa mbali na kuongeza zawadi pia zaidi ya washindi 50 wameshafaidika na promosheni hiyo.

Baadhi ya washindi waliojishindia zawadi ya promosheni hiyo ni Hellen Mbise aliyeshinda simu ya mkononi, Juliaus Mbiduka Sh milioni 2,Isdory Pantras Shmilioni 2,Emanuel Nkumbi Sh milioni 2 na Belinda Kirita Sh milioni 2.

Wakati huo huo washindi wawili wa promosheni ya Fikiria Mazuri walikabidhiwa zawadi zao za Bajaj aina ya Toyo.

Washindi hao ni Aisha Cheyo na Idd Kafterana wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Aisha ambaye alikuwa na furaha iliyomfanya alale chini na kushangilia aliishukuru kampuni hiyo kwa kuweza kumpatia usafiri huo.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.