Habari za Punde

*FANCY NKULI ACHAGULIWA KUGOMBEA UBUNGE KUNDI LA VIJANA MKOA WA SINGIDA

Msimamizi mkuu wa uchaguzi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Singida Pascal Mabiti akimpongeza FANCY baada ya kuchaguliwa kuwania nafasi ya kugombea Ubunge wa kundi la Vijana.
Na Hillary Shoo,
Singida.

KATIBU wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya (UNA) United Nation Asociation iliyopo kwenye jengo la umoja wa mataifa jijini Dare s salaam Fancy Nkuhi (25) amechaguliwa kuwa mmoja wa wagombea Ubunge kundi la vijana kutoka mkoani Singida.
Fancy aliibuka kidedea kwa kupata kura 16 kati ya kura 29 zilizopigwa jana na wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani hapa.
Katika uchaguzi huo mshindi alipata upinzani mkali kutoka kwa msindi wa pili Jamila Hasan aliyepata kura 10 huku Vailet Eliasi ambaye ni mfanyakazi wa ofisi ya UVCCM makao makuu akiambulia kura 3.
Mjasiriamali kutoka Kinondoni Mosi Ntandu aliambulia patupu baada ya kupata kura sifuri.
Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo Fancy mwenye shahada ya sheria kutoka chuo kikuu huria,alisema matarajio yake ni kuhakikisha fursa wanazopata vijana katika nyanja mbalimbali zinafanikiwa.
Alisema atahakikisha kuwa fursa hizo zinapata msimamizi mwenye uwezo wa kuzitetea katika bunge pindi atakapochaguliwa kushika nafasi hiyo.
Hata hivyo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Pascal Mabiti aliwataka vijana hao kuunganisha nguvu ya pamoja na kuvunja makundi ili kuhakikisha mwakilishi huyo kutoka mkoani hapa anaibuka mshindi katika awamu ya pili Mkoani dodoma Agosti 3 mwaka huu.


Fancy, akipongezwa na baadhi ya wanachama na vijana wenzake baada ya uchaguzi huo.

Fancy akiwa na wapiga kura katika picha ya pamoja.

Fancy akipiga picha ya kumbukumbu na mgobea mwenza baada ya kumshinda.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.