Habari za Punde

*ANKAL MICHUZI AFANYA UZINDUZ LAINI WA LIBENEKE JIPYA


TANGAZO, TANGAZO, TANGAZO
MDAU WA SUFIANIMAFOTO PIA WAWEZA KUTEMBELEA LIBENEKE JIPYA LA MICHUZI LILILOZINDULIWA JUZI KUPITIA:- www.michuzipost.com
Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipyala www.michuzipost.com ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katikakile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwakutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanzakabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa.
Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu yalibeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya KuendelezaLibeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyonakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidiakuboresha libeneke hili.
Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kamaujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikionsikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulukwa muda wote huu.
Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaendasambamba na Libeneke hili la
www.michuzipost.com pamoja na lile lawww.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamiiitaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipyaambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwamapana na undani zaidi.
Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmimnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miakamitano kammili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hiiinavyojionesha
http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments.
Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapanilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipasapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeoyangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulanihuko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendeleakama kawa.
Libeneke hili jipya la
www.michuzi.post.com limewezekana kwa ushaurina msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw.Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamojatutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wabidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazikikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libenekehili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.