Habari za Punde

*CHADEMA YASHINDA KITI CHA UBUNGE MUSOMA MJINI

*KINA MAMA WAFUNGIWA NDANI, WASHINDWA KUPIGA KURA.

*VITUO VYA KUPIGIA KURA VYATAWALIWA NA VIJANA.

Mgombea ubunge kwa kiti cha CHADEMA Vicent Kiboko Nyerere, ambaye katika kampeni alikuwa akitajwa kama ’ Vicent Josephat Nyerere’ ameibuka kidedea baada ya kutangazwa kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini kote.

Katika Jimbo hilo la Musoma mjini Vicent ameweza kuibuka kidedea na kutangazwa baada ya kushinda katika kata kadhaa huku mgombea wa CCM, akiibuka na kura kiduchu.

Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu kutoka Musoma Mjini, Mwandishi Eversweet, amesema kuwa asilimia kubwa ya wapiga kura waliokuwapo katika vituo jana walikuwa ni vijana, huku kinamama wakiwa ni wa kuhesabu.

Aidha alisema kuwa katika Jimbo hilo la Musoma mjini kinamama walifanyiwa mchezo mchafu kwa kufungiwa ndani hadi muda wa kupiga kura ulipomalizika, kiasi kwamba hadi nafasi ya urais katika baadhi ya Kata mgombea urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete akionekana kushindwa .

Mwandishi huyo alipojaribu kuzungumza na baadhi ya kinamama waliofanyiwa vitendo hivyo, waliogopa kutaja majina yao kwa kuhofia usalama wao, huku pia wakisema kuwa wameogopa kuripoti tukio hilo katika vituo vya Polisi kwa kuogopa vitisho vya waume zao na wanaume waliotenda vitendo hivyo.

Katika uchaguzi huo CHADEMA imeibuka na jumla ya kura, 21, 335 awa na asilimia 59. 71. CCM imepata jumla ya kura 14, 072 sawa na aslimia 39.38. CUF kura 253 sawa na asilimia 0.71. NCCR kura 19 sawa na asilimia 0.o5. DP kura 53 sawa na asilimia 0.15.
Idadi ya waliojiaikindikisha walikuwa 79, 527 na wapiga kura walikuwa ni 36, 230 na kura zilizoharibika zilikuwa ni 498 na halali zilikuwa ni 35, 732.
Habari zilizopatikana mpaka hvi sasa kuhusu Majimbo yaliyochukuliwa na upinzani ni pamoja na Liwale, Iringa Mjini, Mbeya Lindi mjini, tutaendelea kuwaletea matokeo mengine kadri tutakavyopata matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.