Habari za Punde

*DK. BILAL AFUNIKA PEMBA

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati alipofanya mkutano wa kampeni katika jimbo hilo leo.
Aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa CUF, Juma Othman Juma, akiinua mikono kuwasalimia wananchi wakati alipoalikwa akipanda jukwaani kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Gando, wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa urais wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal, alipofanya mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya Kizimbani leo.
Wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakimsikiliza mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipofanya mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya Kizimbani, leo


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.