Habari za Punde

*DK. BILAL AWAFARIJI WAFIWA NA MAJERUHI WA AJALI-PEMBA

Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akishiriki dua ya pamoja na wananchi wa Kijiji cha Chonga Chake Chake waliofiwa na ndugu zao waliopata ajalia hivi karibuni wakati wakitoka katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Zanzibar, Dk Shein uliofanyika hivi karibuni Konde Pemba. Ajali hiyo iliua watu 5 na kujeruhi 29 ambao wamelaza katika Hospitali ya Chake Chake.
Dk. Bilal, akiingia Hospitali ya Chake Chake kuwatembelea Majeruhi wa ajali hiyo...
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji mtoto, Mwanaidi Yazid Mohamed (2) ambaye ni miongoni mwa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Chake Chake Pemba, baada ya kupata ajali baada ya gari lao kupinduka lilipokuwa likitoka kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika Konde Pemba hivi karibuni. Katika ajali hiyo walifariki watu 5 na 29 kujeruhiwa, ambao wote wamelilazwa katika Hospitali hiyo. Kushoto ni Mama mzazi wa mtoto huyo, Nipe Salum.
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimpa pole Masoud Hamis Mbarawa, mkazi wa Kipapo, aliyelazwa katika Hospitali ya Chake Chake Pemba, baada ya kupata ajali baada ya gari lao kupinduka lilipokuwa likitoka kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika Konde Pemba hivi karibuni. Katika ajali hiyo walifariki watu 5 na 29 kujeruhiwa, ambao wote wamelilazwa katika Hospitali hiyo.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.