Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe iiwa ni ishala ya kukalibishwa katika Wilaiya ya Ilemela Mkoani Mwanza wakati alipowasili wilayani hum oleo Okt 22 kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo, Anthony Dialo. 
Dk. Bilal akisalimiana na baadhi ya Makada wa CCM wa Wilaya ya Ilemela baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Buzuruga kufanya mkutano wa kampeni leo.
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea kadi za wananchama wa Vyama vya upinzani 128 walioamua kujiunga na CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Buzuruga Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza leo.
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akionyesha sehemu ya 128 ambazo ni kadi za wananchama wa vyama pinzani waliozirejesha na kumkabidhi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Buzuruga Jimbo la Ilemela na kuwakabidhi kadi mpya za CCM leo. 
Waziri Lawrance Marsha, akizongwa na wananchi na hasa vijana, wakati akitoka kwenye mkutano wa Mgombea Mwenza Dk. Bilal, huku kila mmoja akitaka angalau kumshika mkono na huku wakimwambia kuwa wanamuhitaji awatembelee siku maalum katika Wilaya yao ya Ilemela.

Hapa kila mmoja akijaribu kuwahi kumshika mkono na wengine kila mmoja akimueleza shida yake...
"Ohooooooooo, Ishakuwa Taabu sasa wacha nisepe kiaina hapa"

Hapa akijaribu kuwatoka na kuondoka zake kuwahi gari....

Wananchi waliofurika katika mkutano Dk Bilal, wakitawanyika baada ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment