Mama mzazi wa binti huyo Salome kapele ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Izia alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 usiku wakati binti yake huyo akitoka kupata mbili tatu katika klabu ya pombe za kienyeji (yaani kunywa pombe ya kienyeji).
Aidha alisema kuwa akiwa amelala aligongewa mlango wa wasamaria wema kumjulisha juu ya tukio hilo la kuvamiwa kwa binti yake huyo japo hakuweza kutoka nje kwa kuhofu usalama wake kutoka kwa wavamizi hao .
“Kweli siku ya tukio kuwa vijana walikuja kunigongea mlango wangu na kunieleza kuwa mtoto wangu anapigwa ila sikuweza kutoka kwani niliogopa iwapo ningetoka……baada ya hapo alikuja kijana mwingine na kunieleza kuwa mtoto wangu amekatwa ulimi baada ya kung’atwa ulimi laikini mie sikuweza sikutoka hadi alipokuja mume wake ndipo nilitoka na kwenda kumkuta akiwa hoi”
Binti huyo kwa sasa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkowa Rukwa akiendelea kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment