*WAUGUZI WATUMIA SIMU ZA TOCHI KUWAHUDUIA WAGONJWA
*NDUGU WATUMIA MISHUMAA KUONA WAGONJWA WAO
Wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa leo walihaha kunusuru maisha yao baada ya jengo zima kukosa umeme kwa muda wa saa moja kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2.20 usiku kutokana na umeme wa shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kukatika bila taarifa.
Hali hiyo ambayo imesababisha kizaa zaa kikubwa katika Hospitali hiyo imeelezwa kutokea baada ya Jenereta ya Hospitali hiyo ambayo kwa kawaida hutumika pale umeme unapokatika nayo kushindwa kufanya kazi.
Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa kuutokana na umeme kukatika na jengo hilo kuwa gizani wauguzi walilazimika kutumia tochi za simu zao huku wengine wakitumia mishumaa kuona wagonjwa wao.
Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Iringa Dk.Ezekiel Mpuya alipoulizwa na mwandishi wa mtandao huu kwa njia ya simu amethibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kuwa tatizo hilo limetokana na umeme wenyewe na kuwa mafundi wa Tanesco tayari wamejulisha juu ya hali hiyo huku Jenereta la Hospitali hiyo akidai kuwa ni bovu

No comments:
Post a Comment