Habari za Punde

*SIMBA MDEBWEDO KWA YANGA, YACHAPWA 1-0

"NENDA KAWAONYESHE KUWA HAPA NI HOME KWENU SI UNACHEK NDUGUZO WALIVYOKUJA KUKUDEKU? USIFANYE MAKOSA.....NAKUAMINIA........" Kocha Mkuu wa Yanga akimuelekeza jambo mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete, wakati akijiandaa kuingia uwanjani na kufanya kweli.
Kamisaa wa mchezo huo akimuamuru Kocha wa Yanga Papic, kutoka nje ya uwanja wakati mchezo huo ukiendelea..
Ilikuwa ni Raha tuuuuu kwa Jerry Tegete, baada ya kuitungua Simba kwani hapa ni nyumbani kwao hivyo aliwapa raha kamili washkaji, ndugu na jamaa ama kwa hakika ilikuwa ni zawadi tosha kwa nduguze wa Mwanza..
Golikipa wa Simba Juma Kaseja akijiandaa kudaka mpira ili kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga Nsa Job wakati wa mchezo huo.
Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa 'Fuso' akimkwatua Emmanuel Okwi wakati wa mchezo huo..
Mashabiki wa Yanga wakiwa na jezi wa Jerry Tegete....

PATRIC PHILL HOI KWA PAPIC
Timu ya Dar Young African ya Jijini Dar es Salaam, ls Clueo imeibuka kidedea baadbuliaji a ya kuwachapa watani wao wa jadi Simba Sport bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ambao umemalizika muda mchache uliopita.
Goli hilo limefungwa na mshambuliaji machachari Jerry Tegete katika dakika ya 67 ya mchezo kufuatia pasi nzuri ya Nsa Job.
Katika mchezo huo Simba iliweza kutawala mchezo katika dakika za mwanzo huku Yanga wakiutawala mchezo huo katika dakika zote za kipindi cha pili.
Naye Kocha wa Yanga Papic alitolewa nje ya uwanja na mwamuzi wa mchezo huo. Na huu ni ushindi wa 4 kati ya mechi 8 zilizochezwa kwenye uwanja huo, ambapo Simba imeshinda mara 2, na ikatoa droo 2

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.