Habari za Punde

*BI KIZEE AMPA BARAKA ZA KUWA MAKAMU WA RAIS DK BILAL

Mgombea mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Garib Bilal, akisalimiana na kupewa baraka na Bibi Marcerwag Ndwala mkazi wa Kijiji cha Manyara Kibaoni Wilaya ya Karatu, wakati Dk. Bilal aliposimama katika kijiji hicho kusalimia wanakijiji akiwa safarini kuelekea Kijiji cha Mbulumbulu, ambapo Bibi huyo alimbusu mkononi ‘kumtemea mate’ ikiwa ni ishara ya kumtakia mema kufanikisha ushindi wa kishindo baada ya kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Wananchi na wanachama wa CCM wa wilaya ya Monduli wakimpokea Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiingia Wilaya hiyo katika Jimbo la Edward Lowassa jana kufanya mkutano wa kampeni.
Dk Bilal akipunga mkono kusalimia wananch...
Mbunge Mteule Mtarajiwa wa Viti Maalum wa Mkoa wa Arusha akiwa ni miongoni mwa watu waliokuwapo katika mkutano huo..
Sufianimafoto akipiga picha ya kumbukumbu na Wanamama wa Kabila la Kimasai wa Wilaya ya Monduli, waliokuwapo katika mkutano huo wa Dk Bilal.
Maeneo haya usafiri wa kurejea majumbani katika vijiji jirani na eneo la mkutano ilikuwa ni mbinde....



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.