Ajali hii imetokea saa 2.20 usiku wa jana eneo la Ruco jirani na Benki ya NMB mjini Iringa katika barabara kuu ya Dodoma -Iringa ama Kihesa -Posta ambapo Taxi hiyo iligongwa wakati ikijaribu kuingia upande wa pili wa barabara kuelekea barabara ya Ikulu Ndogo eneo la Gangilonga.
katika ajali hiyo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Kalinga ambaye anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 50, aliyekuwa mlemavu ambaye pia ni mfanyakazi katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, aliyekuwa abiria katika gari hilo amefariki papo hapo.
Dereva wa Taxi hiyo alikamatwa na polisi japo taxi hiyo ni mali ya mmoja kati ya askari wa usalama barabarani mjini Iringa huku daladala iliyosababisha ajali hiyo ikitoweka ,Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment