Habari za Punde

*VITUKO VYA ASKARI WA USALAMA BARABARANI, KAZI NA DAWA

Askari wa usalama Barabarani, akitimua mbio wakati akiwa bize kuongoza magari kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Nyerere eneo la Keko. Askari huyo alimuacha hio kila aliyekuwapo eneo hilo kwa jinsi alivyokuwa akionyesha mikogo yake wakati akiongoza magari. Ama kwa hakika kila aliyekuwa eneo hilo aliburudika na wala hakutamani aruhusiwe haraka kwa burudani hiyo iliyokuwa ikitolewa na afande huyo, na hata aliyekuwa na haraka na akakwama eneo hilo katika foleni basi hasira zilimwishia na naamini wengi walitamani foleni hiyo iendelee kwa upande wake ili aendelee kupata burudani, kwani hata mie nilikuwa naelekea Uwanja wa Uhuru katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa kati ya Kilimanjaro na harambee lakini sikuona kama nazidi kuchelewa. Aiweka pozi kwa kukunja Nne wakati akiwa katikati ya barabara akiendelea na kazi hiyo.
akionyesha ishara ya saa kuashiria madereva kutopoteza muda ili waweze kuongeza mwendo kuwahi kupita eneo hilo kuepuka foleni.
Akiamuaru magari ya upande wa pili yanayotokea Ilala kupita, huku madereva wa pikipiki na magari nyuma yake wakivunjika mbavu kwa vituko vyake, ama kwa hakika ilikuwa ni burudani tosha mahala hapo kwa siku hiyo kuzidi hata ya Twanga Pepeta.
Haya twendeeeee, akiyaita magari....





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.