Habari za Punde

*SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI LA DANCE MUSIC COMPETITION KUANZA DES 20 DAR

Mkurugenzi wa Makukwe Entertainment, Suleiman Mathew, akizungumza na waandsihi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu shindano la kusaka vipaji vya kuimba muziki wa dansi ‘Dance Music Competition’, linalotarajia kuanza jijini Dar es Salaam Desemba 2o katika Wilaya ya Kinondoni na baadaye Wilaya ya Ilala na Ilala. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Asha Maulid (kulia) ni Mwimbaji wa bendi ya Extra Bongo, Emmanuel Michael ‘Bob Kissa’.
Na Mwandishi wa Sufianimafoto
SHINDANO la kusaka vipaji vya waimbaji wa
muziki wa dansi nchini,kuanza Desemba 20 na
kukamilika mwezi wa tatu mwakani.
Shindano hilo lililoandaliwa maalum kwa ajili
ya kutafuta na kuibua vipaji vya vijana wenye
uwezo wa kuimba aina hiyo ya muziki, pia
linamalengo ya kukuza vipaji vya wasanii hao
ambao wengi wamekuwa wakishinda jinsi ya
kuibuka na kujitambulisha katika jukwaa la
muziki wa dansi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makwekwe
Entertainment, Suleiman Mathew, alisema kuwa
katika shindano hilo, vikundi mbalimbali
vitachuana kuwania taji la kundi bora nchini.
“Tumeona tushiriki kukuza na kuendeleza
vipaji vya vijana wetu, kwa kupitia muziki wa
dansi nchini, muziki ambao unakimbiwa na
vijana wengi ambao hukimbilia katika Bongo
Fleva", alisema Mathew.
Aidha alitaja ratiba ya mchakato huo kuwa, Desemba 20 na 21 saa 4 hadi saa 10 za jioni,
usaili wa wanamuziki hao utafanyika Rufita
Baa, Sinza Mori katika Wilaya ya Kinondoni, Na
Ilala wao utafanyika katika Ukumbi wa DDC
Kariakoo, Desemba 23 na 24 muda ule ule, huku
Temeke ukifanyika katika Ukumbi wa Ikweta
desemba 27-28.

Wasanii wanaounda kikundi cha ‘New Young Music’, wakiimba kwa pamoja wimbo wa bendi ya Msondo, wakati wa mkutano wa utambulisho wa shindano la kusaka vipaji vya waimbaji wa muziki wa Dansi, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Zoezi hilo la kusaka vipaji linatarajia kuanza Desemba 20 katika Wilaya ya Kinondoni kwenye Ukumbi wa Rufita Sinza na baadaye Wilaya ya Ilala na Temeke

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.