Habari za Punde

*CHADEMA WAMTEUA MPINZANI WA NDUGAI KUWANIA KITI CHA NAIBU SPIKA WA BUNGE

Mh. Mustapha Akonay-CHADEMA
Kwa upande wake, CHADEMA
imemteua Mbunge wake wa jimbo la Mbulu, Mustapha Akonay, kuwania unaibu spika.

MBUNGE wa Kongwa, Job Ndugai
Uchaguzi wa Naibu Spika wa Bunge utafanyika Jumanne , ambapo jana majira ya saa 10 jioni ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wagombea wa nafasi hiyo katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alisema kuwa, mkutano wa Kamati ya Wabunge wa CCM imempa ushindi wa kishindo Ndugai, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Chiligati alisema hadi jana jioni, wanachama watatu wa CCM walijitokeza kuwania nafasi hiyo, ambao ni Ndugai, Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na Mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu.
Alisema wakati wa mkutano jana, Dk. Limbu alitangaza kuondoa jina lake kwenye kinyang’anyiro hicho, akisema hana sifa kama walizonazo wagombea wenzake.
Kwa mujibu wa Chiligati, Jenista, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge lililopita alipokuwa akijieleza mbele ya wagombea, alisema anaondoa jina lake, hivyo asipigiwe kura.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.