Habari za Punde

*CHENGE, MAKINDA NAO WACHUKUA FOMU KUCHUANA NA S.SITTA

Aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge na Anne Makinda aliyetetea Kiti chake cha Jimbo la Njombe Mashariki, nao wamejitokeza kuchukua fomu na kutangaza rasmi kuwania Kiti cha Spika wa Bunge lijalo la Jamhuri ya Tanzania.
Machachari hao wamechukua fomu jana na kuomba kuteuliwa na chama cha mapinduzi, ili kuwania nafasi hiyo ambayo pia badi inatetewa na na aliyeishikilia katika kipindi kilichopita Samuel Sitta.
Sitta ambaye amekuwa spika kwa miaka Mitano amechukua fomu kutetea kiti hicho, baada ya kushinda kiti cha ubunge katika jimbo la Urambo Mashariki.
Kwa upande wake Makinda, ambaye anamaliza muda wake wa unaibu spika, ambaye amekuwa mbunge wa Njombe Mashariki kwa muda mrefu, naye ameweza kutetea kiti chake kwa kupita bila kupingwa.
Mkuu wa kitengo cha uchaguzi, Mattson Chizzi amesema fomu hizo zimeanza kutolewa tangu juzi, na kuwa wanachama wengine wanatarajiwa kuchukua fomu hizo za kuwania uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hii leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.