Habari za Punde

*ALIYEDAIWA KUUAWA ZANZIBAR, AIBUKIA GEZENGA AKIUZA MAFAGIO KAMA KAWA

Hivi karibuni mjini Zanzibar ulizuka uvumi kuwa mfanyabiashara maarufu wa mafagio na vifaa vya kupikia katika mitaa ta mjini Zanzibar, Kibonge Seme (50) kuwa amefariki kwa kunyongwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa kwenye eneo la ufukwe wa Kizingo mjini Unguja. Pichani ni mfanyabishara huyo, Kibonge, akizungumza na wakazi wa mtaa wa Gizenga mjini Zanzibar ambao kwa mshangao mkubwa hawakuamini macho yao baada ya kumwona akiwa katika kazi yake iliyompa umaarufu, huku akiendelea na kazi hiyo ya kuuza fagio na vifaa vingine vya nyumbani leo mchana, kiasi kwamba watu wengine waliweza kutimua mbio mara tu baada ya kumuona wakizani kuwa ni mzimu wake, na kumuacha yeye akibaki kuwashangaa. Kibonge alishangaa na kutojua sababu za uvumi huo, hata hivyo alielezea kuwa kwa mwezi mmoja ulopita alisafiri kwenda Tanzania Bara kusalimia ndugu zake na kumalizia kuwa yeye ni mzima wa afya.Picha na Martin Kabemba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.