Katik hafla ya kutangaza matokeo ya Urais iliyomalizika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame, ameweza kutoa majumuisho ya matokeo hayo na kutangaza rasmi kuwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, ameibuka mshindi kwa kupata Asilimia 67.17 na n ameteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano. Makame alisema kuwa Rais Kikwete ameibuka mshindi baada ya kupata jumla ya kura Milioni 5, 276, 827 ambayo ni sawa na asilimia 61.17 % ya watu wote waliopiga kura, na kufuatiwa na mpinzani wake Dk Willbroad Slaa kupitia chama cha CHADEMA, ambaye ameibuka na jumla ya kura Mil.2, 271, 941 ambayo ni sawa na asilimia 20% ya wapiga kura. Ambapo jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa ni Milioni 20, 137, 303, wakati walijitokeza kupiga kura walikuwa ni Milioni 8, 6261.283 ambayo ni 42% ya waliopiga kura.
Wagombea wengine ni pamoja na
1:- KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO - 1.12%2.
2:- KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM - 5, 76,827 61.17%
3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA - 2,271,942 26.34%
4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF - 695,667 8%
5. RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 26,388 0.31%
6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 17,482 0.20%
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 13,176 0.15%,
.

No comments:
Post a Comment